INPS Japan
HomeLanguageSwahiliKwa nini kutumia dollar thelathini kwa mwaka kwa kila...

Kwa nini kutumia dollar thelathini kwa mwaka kwa kila kijana ni muhimu

Imeandikwa na J Nastranis

NEW YORK (IDN) – Kulingana na utafiti wa tume ya UNFPA, United Nations Population Fund, utumizi wa chini ya dola thelathini kwa kila mtu kwa kila mwaka unaweza kufanya maajabu kwa afya na elimu ya vijana .

Ripoti imechapishwa kwa Lanceti siku moja kabla ya mikutano ya World Bank Spring mjini Washington D.C.kuanzia mwezi wa Aprili 21 hadi Aprili 23, 2017, ambapo viongozi wa kifedha na maendeleo kutoka nchi 188 wamepangiwa kuchangia umuhimu wa kuwekezea vijana .

Lanceti ni jarida la ujumla la kimatibabu la kimataifa la kujitegemea lenye limesemekana kufanya sayansi ipatikane kwa urahisi kila mahali ili dawa zitumike kutumikia na kubadilisha jamii ,na kuchangia ipasavyo kwa maisha ya watu.

Utafiti ulifanywa siku chache baada ya uamuzi wa nchi ya Marekani kukatiza mchango wa kifedha kwa shirika la UN Population Agency. Huu ndio ukomeshaji wa kwanza wa mchango wa kifedha wa Marekani kwa shirika la UN uliotangazwa na Rais Donald Trump. Hati, inayonukuu marekebisho ya Kemp-Kasten –iliyopitishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1985 na kutumiwa awali na rais wengine wa kiripablika– inadai kua shirika la UNFPA “limesaidia, au kushiriki katika usimamizi wa mpango wa utoaji mimba kwa kilazima au kutasishwa bila kujitolea” katika nchi ya China.

Marekebisho yamekataza kupeana kwa msaada wa kigeni kwa shirika lenye limejihusisha kwa utoaji wa mimba kwa lazima au kutasishwa bila kujitolea. Maraisi Ronald Reagan, George HW Bush na George W Bush walikataa kupeana hela kwa shirika la UNFPA kwa sababu hiyo hiyo. (Soma U.S. Reasoning Behind Cutting Funds to UNFPA Challenged)

Kulingana na utafiti ,kuboresha afya ya kimwili, kingono na kiakili ya vijana kati ya miaka 10 hadi 19, inaeza kuepusha vifo zaidi ya million 12 za vijana na zaidi ya million thelathini ya mimba zisizotakikana ,.

Vile vile, mipango za kupunguza ndoa za utotoni, kama dola 3.80 kwa kila mtu, inaeza kuleta mara sita kurudi juu ya uwekezaji na kukata ndoa za utotoni na karibu thuluthi tatu.

Mkurugenzi mtendaji Dr Babatunde Osotimehin wa shirika la UNFPA alisema kuwa uwekezaji kwa vijana ni hamu wa muda mrefu wa kila mtu na maslahi ya kimkakati,. “Uwekezaji ndogo katika kuwezesha na kulinda vijana zaidi ya billion moja duniani inaeza kuleta mara kumi kurudi au wakati mwingine zaidi. Uanzilishi utafiti wetu lazima uonekane na watengeneza sera, na utumike kuchati dunia mbele.”

Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Victoria nchini Australia, Chuo kikuu cha Melbourne, na shirika la UNFPA ndizo zilizoongoza katika utafiti. Wahandisi walihesabu athari za kifedha na kijamii kwa mwingilio wa kiafya kwa kuboresha huduma za afya kwa vijana na kupanua chanjo zaa HPV (Virusi vya Papilloma kwa binadamu), miongoni mwa zingine . Pia wanahesabu athari za mipango za kupunguza ndoa za utotoni na vurugu kati ya wapenzi, kuboresha mahudhurio ya shule na ubora wa kielimu.

“uwekezaji bora zingine kwa afya na ustawi wa vijana unapatikana nje ya sekta ya afya– kupambana na ndoa za utotoni, kupunguza majeruhi ya barabara na kuboresha elimu,” asema mhandisi mkuu Peter Sheehan, kutoka chuo kikuu cha Victoria.

“Kuna shaka kidogo ya kuwa matendo yalivyoainishwa katika utafiti wetu yanaweza kuwekwa mikononi kwa kiasi kikubwa katika nchi ya kubadilisha maisha ya wavulana na wasichana katika dunia nzima. Athari za kifedha na za kijamii za uwekezaji juu ya afya na ustawi wa vijana ziko juu kwa viwango yoyote na ziko katika uwekezaji bora zaidi yenye jumuia ya kimataifa inaeza fanya kufikia malengo ya maendeleo ya shirika la UN.

Ripoti inakisia kua gharama ya jumla hadi mwaka 2030 ya hatua zote zilizochunguzwa, kwa dola bilioni 524 , sawa na 6.70 kwa kila dola kwa mtu kwa kila mwaka isipokua kwa elimu. Kwa elimu , kwa jumla inakisiwa kua dola trilioni 1.77 au dola 22.60 kwa kila mtu kwa kila mwaka.

Kuchukuliwa kwa pamoja , bei itakua chini ya dola , 30 kwa mwaka kwa kila mtu . kwa Ujumla, uwekezaji wa mwaka katika mipango yote itakua sawa na asilimia 0.20 ya pato la dunia. [InDepthNews – 20 April 2017]

Picha: Wasichana kutoka Safeguard Young People programme ya Malawi, yenye inatoa taarifa ya afya ya uzazi na kujamiiana , inasaidia vijana kupata huduma za kiafya, na kupatiana mafunzo ya kiongozi. Chanzo: UNFPA Malawi/Hope Ngwira.

Most Popular