INPS Japan
HomeLanguageSwahiliCOVID-19 Inasitisha Elimu Kusini mwa Afrika

COVID-19 Inasitisha Elimu Kusini mwa Afrika

Na Jeffrey Moyo

MUSINA, Afrika Kusini (IDN) – Watoto wake watatu wa ujana hucheza mpira wa karatasi uliotengenezwa nyumbani kwenye barabara zenye vumbi za Musina, vitabu vya kuandika vimetawanyika kwenye varanda ya nyumba yao ya kukodi katika mji wa mpakani mwa Afrika Kusini na Zimbabwe. Walakini Gerald Gava, baba wa watoto mwenye umri wa miaka 47, hulala kwenye mkeka uliotandazwa kwenye varanda, inavyoonekana hana chochote cha kufanya baada ya kuacha kufanya kazi miezi mitatu iliyopita wakati kuzuiliwa kuliathiri kampuni ya ujenzi iliyomuajiri.

Gava, ambaye ni mhamiaji kutoka Zimbabwe, alisema hata watoto wake wamelazimika kubaki nyumbani kwani shule pia zimefungwa, kwa sababu ya virusi vya korona ambavyo vimepiga dunia nzima.

Sasa, mke wa Gava mwenye umri wa miaka 42, Mirirai amekuwa wa kutegemewa wa pekee, anaendesha kibanda cha sokoni kando ya barabara karibu sana na nyumba yao, kazi ambayo alikuwa ameiacha mwanzo nchini mwao hadi walipotafuta maisha bora nchini Afrika Kusini.

Lakini maisha sio bora tena.

Huku elimu ikisitishwa na virusi vya korona kote Kusini mwa Afrika, watoto wa Gava wako miongoni mwa mamilioni ya watoto wanaokwenda shule ambao elimu yao imevurugwa na janga la COVID-19.

“Ninaweza kukuambia kuwa hata ninapowalazimisha watoto wangu kusoma peke yao, wamechoka na wamegeuka kucheza michezo kwa sababu kisitishwa kwa shughuli za kawaida kumechosha sana,” Gava, aliyehitimu ualimu kutoka nchini mwake, aliiambia IDN.

Hadithi ni hiyo hiyo nchini Zimbabwe, ambapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanabaki manyumbani mwao huku matarajio yakipungua haraka kwamba watawahirudi shuleni wakati wowote kwani visa vya virusi vya korona vinazidi Kusini mwa Afrika.

Kwa wazazi wengi wa Zimbabwe kama Miranda Mutasa mwenye umri wa miaka 31 katika eneo la Harare lenye wiani mkubwa wa Mufakose katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare, masomo ya nyumbani na hata ujifunzaji mtandaoni hawezi kufikia.

Walakini, virusi vya korona vinapositisha elimu eneo kote hapa, katika barua ya pamoja na UNICEF kwa mataifa wanachama wake, Umoja wa Afrika (AU) mnamo Juni mwaka huu ulishinikiza ustahimilivu ili kuwafanya wanafunzi wajiendeleze na masomo yao wakati wa kusitishwa kwa shughuli za kawaida. “Kutoa masomo ya mbali, kusambaza redio, TV, yaliyojiri na kujifunza mtandaoni,” soma sehemu ya barua.  

Barua ya AU-UNICEF pia ilisema: “Wizara za Elimu zinapaswa kutayarisha mazoea mazuri na kufuatilia ushiriki wa ujifunzaji na matokeo ya kujifunza ili kuboresha jibu la sekta ya elimu kwa COVID-19.”

Lakini, kwa Waafrika Kusini wengi kama Gava sasa wamekosa kazi, kwa mfano, kusoma kwa njia ya kielektroniki, labda ni ndoto ndefu hata wakati AU inashinikiza njia hii haswa kuhakikisha mwendelezo katika elimu.

Kwa walimu waliostaafu nchini Zimbabwe kama Bernard Mungoni mwenye umri wa miaka 72 aliyeko Masvingo, mji mkongwe zaidi nchini, kusini mwa nchi, “virusi vya korona vimeanzisha gharama mpya ambazo wengi hawawezi kumudu”.

Miranda, anayefanya kazi kama muuzaji wa barabarani anayeuza matunda na mboga, alisema, “Vifurushi vya mtandao ili kupata vifaa vinavyohitajika vya kujifunzia kwa watoto wake, ni ghali mno”.

Vile vile, kwake (Miranda), virusi vya korona vimesimamisha masomo nchini mwake, na kuwaacha watoto wake katika hali mbaya.

Visa vya janga la COVID-19 vinaposambaa Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika kupitia usimamizi wake ilikubali kufanya kazi na UNESCO, ikiongoza Muungano wa Elimu Duniani kusaidia Mataifa Wanachama wa SADC katika kupunguza athari za virusi vya korona juu ya elimu, na katika kuhakikisha mwendelezo wa mipango ya elimu na ujifunzaji.  

Sasa, zikiwa zimekabiliwa na virusi vya korona, nchi kama Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe na Namibia zinabeba mzigo wa janga hilo kwa watoto wa shule. Hali hii imelazimisha nchi hizo kuwa na wazo la pili juu ya kufunguliwa kwa shule. 

Nchini Angola, kuanzia Machi tarehe 24, maumivu ya kuenea kwa virusi vya korona, serikali ya Angola ilitangaza kukatizwa kwa masomo katika shule za umma na za kibinafsi. Wizara ya Elimu ya Angola iliingia kwenye rekodi katika vyombo vya habari ikisema kusimamishwa kwa shughuli za kielimu kote nchini kulifuatana na maagizo yaliyotolewa na serikali kuhusu hatua za kujikinga dhidi ya virusi vipya vya korona. 

Nchini Uswazi, mnamo Machi, virusi vya korona viliposhambulia, Chama cha Kitaifa cha Walimu cha Uswazi (SNAT) kilihimiza serikali kufunga shule zote, vyuo na vyuo vikuu kwa muda

Katika taarifa, chama cha walimu cha Uswazi kilisema, “SNAT ina wasiwasi juu ya ukweli kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa kupambana na hili tisho, haswa katika maeneo ya umma kama miji, majiji na shule”.

Nchini Botswana, virusi vya korona vilipopiga Kusini mwa Afrika mapema mwaka huu, nchi hiyo ilifunga shule wiki saba kabla ya kufunguliwa kwa shule mnamo Juni na mara moja ikafunga tena katika maambukizi mapya ya ugonjwa huo wa kutisha.

Akitangaza kusitishwa tena kwa shughuli za kawaida awali mnamo Juni, waziri wa afya wa Botswana, Dk Lemogang Kwape alisema: “Ninasikitika kuwajulisha kuwa hali imekuwa mbaya zaidi katika masaa 24 yaliyopita. Botswana imeandikisha visa 30 vipya vya COVID-19, na visa vingi vinavyotoka shule katika Gaborone kubwa”.

Kwa kufungwa kabisa na kuenea kwa virusi vya korona ambavyo havijaepuka shule zake, Afrika Kusini mnamo Julai pia ilitangaza kwamba shule zinaendelea kufungwa, hii ni kwa sababu serikali itasongesha mwaka wa shule wa 2020 ndani ya 2021.

“Tumechukua njia ya makusudi kufunga shule wakati ambapo nchi inatarajiwa kupata ongezeko kubwa la maambukizi,” alisema Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia taifa mnamo Julai.

Kugeukia Namibia, mnamo Agosti tarehe 1 mwaka huu, Rais wa nchi hiyo Hage Geingob alitangaza kuwa serikali yake inasitisha shule kutoka Agosti tarehe 4 kwa siku 28, akisema hatua hiyo ni muhimu ili kuondoa hatari zinazohusiana na kuenea kwa virusi vya korona. 

Huku COVID-19 ikivuruga sana elimu hapa, mnamo Machi tena mwaka huu, Wizara ya Elimu ya Namibia ilikuwa imefunga shule kwa mara ya kwanza kufuatia kuthibitishwa kwa visa viwili vya COVID-19 katika moja ya shule za umma za nchi.

Nchini Malawi, kuongezeka kwa visa vya COVID-19 mnamo Julai kulilazimisha mamlaka kuchelewesha mipango ya kufungua shule.

Sasa, shule zikiwa zimefungwa Afrika Kusini, kwa mfano, ina maana kwamba Gava na familia yake wanapaswa kubeba mateso na ukiritimba pamoja.

“Watoto wangu wamechoka hapa nyumbani; mimi pia nimechoka, lakini pia ninateseka kwa sababu nimepoteza kazi yangu kwa sababu ya COVID-19,” Gava aliiambia IDN. [IDN-InDepthNews – 18 Agosti 2020]

Picha: Huku kusitishwa kwa shughuli za kawaida kukizuia kuenea kwa COVID-19, Waafrika Kusini wengi, wamepoteza kazi zao na wamegeukia kuuza barabarani ambapo wanakabiliana na polisi wanaotekeleza sheria za kusitisha shughuli za kawaida. Kwa hivyo, mchezo wa kuishi bado unabaki kuwa mgumu kwa Waafrika wengi wanapambana kusaidia watoto wao wakati wa kufungwa kwa shule. Hisani: Jeffrey Moyo | INPS-IDN

Most Popular